Omba Huduma za Bila Malipo za Tafsiri, Mkalimani, au Marekebisho Yanayofaa
Idara ya Kodi ya Vermont imejidhatiti kutoa upatikanaji sawa kwa huduma zetu kwa watu wenye ulemavu. Hii ni pamoja na wale ambao ni Viziwi au wasiosikia vizuri au wenye upungufu wa hisia mbili, pamoja na wale ambao wana uwezo mdogo wa kuongea, kusoma, kuandika au kuelewa Kiingereza.
Omba Mkalimani au Tafsiri
Ikiwa Kiingereza sio lugha yako ya msingi au una uwezo mdogo wa kusoma, kuzungumza, kuandika au kuelewa Kiingereza, una haki ya kupata mkalimani. Idara ya Kodi ya Vermont itakupa mkalimani ili kukusaidia kufikia kodi na programu za Vermont.
Omba Marekebisho Yanayofaa
Walipa kodi wanaweza kuomba marekebisho yanayofaa mapema mtandaoni, kwa simu, kwa maandishi, au ana kwa ana wakati wa miadi yao. Katika ukumbi wa jengo letu na kwenye tovuti yetu, tunachapisha taarifa kuhusu huduma za mkalimani, Kitambulisho cha Lugha, na ishara ya ‘Siwezi Kukusikia’ (‘I Cannot Hear You’) mahali panapoonekana.
Tunajitahidi kufanya mchakato wa ombi la marekebisho uweze kupatikana na kuwafaa watu wote.
Machaguo ya Kuomba Msaada
- Ana kwa ana - Tembelea ukumbi wa jengo letu, na mfanyakazi atawasilisha ombi kwa ajili yako.
- Barua pepe - Tuma ujumbe kwenda tax.support@vermont.gov
- Simu - Piga 802-828-3763
Fomu ya Mamlaka ya Mwanasheria
Madhumuni ya fomu hii ni nini? Unaweza kumteua mtu mwingine, kama vile mtaalamu wa kodi, wakili, mwanafamilia au rafiki kuwa "wakala" wako kwa kutumia fomu hii. Wakala ameidhinishwa kukuwakilisha katika mazungumzo na Idara ya Kodi ya Vermont na kuwasilisha ritani ya kodi kwa niaba yako.
Fomu ya Idhini ya Kutoa Taarifa za Kodi
Madhumuni ya fomu hii ni nini? Fomu hii inaruhusu kupewa mtu mwingine taarifa zako za kodi. Huyu anaweza kuwa mtaalamu wa kodi, wakili, mkalimani, mwanafamilia, au rafiki. Inairuhusu Idara ya Kodi kuzungumza na mtu huyu kuhusu kodi zako.